FAIDA YA KUWA NA WEBSITE YA UTALII

Je umekua ukisikia tuu swala la kuwa na website lakini hujaelewa kwanini haswa uwe na website kwa ajili ya biashara ya UTALII? Au unayo website lakini haujaona bado faida za kuwa na website ? Basi makala hii itakupasha faida haswa ya kuwa na website kwa namna ambayo pengine hujawahi kufikiria.
Hakuna wakati ambao website ni ya muhimu kama wakati ambapo tupo katika zama za utandawazi. Yawezekana ukajiona kuwa unachofanya ni kidogo hivyo hauhitaji website , hata hivyo kuna mengi utakua unakosa kwa kutokujikita katika kuwa na website kwa biashara au asasi yako.
Kukipa thamani ufanyacho
Imekua kawaida watu wengi kuamini kuwa biashara yenye website basi itakua makini . Hata hivyo sio tuu website ili mradi website. Unatakiwa uwe na website ambayo kweli inaonyesha umakini na ubora wa biashara yako ya utalii, hii inajumuisha website yenye muonekano mzuri, yenye maelezo yaliyokamilika, yenye taarifa ambazo kweli na yenye package za utalii zinazouzika.
Kuleta ushawishi
Unahitaji website ili kuweza kujenga uaminifu na kuonekana kweli upo serious haswa kwenye tasnia ya utalii. Website yako itakupa nafasi ya kuwaeleza watu kwa umakini na kwa ushawishi kile unachofanya na kwanini wakutafute wewe. Tena website itakusaidia kufanya ushawishi huu kwa watu wengi sana kuliko kuwa tuu na page za facebook na Instagram ambavyo utasambaza post kwa watu wachache.
Kuelezea Ufanyacho
Website hukufanya uwe na nafasi ya kueleza mambo uyafanyacho kwa watu wengi zaidi. Ni kweli unaweza kuwa na akaunti nyingi za mitandao ya kijamii . Lakini watu wengi hawatopata kukufahamu vizuri kama sio kupitia kwa website yako ambapo utakua na kurasa zilizopangiliwa vema kabisa.
Kupatikana wakati masaa 24 siku 7 za wiki
Ofisi yako hufungwa , lakini website yaweza kupatikana masaa 24 siku 7 za wiki. Hivyo kuwa na website ni fursa kwako kuwafaikia walengwa wako masaa yote kila siku na kukupata kwa haraka zaidi.
Kuwasiliana na kuwaelimisha wateja
Kwa kutumia blog itakayoambatana na website yako utaweza kuwapatia wateja wako na wale wateja watarajiwa Makala ambazo zitawaelimisha na kuwavuta karibu na wewe. Pia ni nafasi yako ya kuwapa updates kuhusu utalii wa hapa Tanzania au mabadiliko mengine ya kiutendaji ya hali ya hewa huko porini, kimarketing na sera za biashara.
Kuwa na email address binafsi
Website itakufanya uweze kuwa na email address inayotaja jina la biashara yako. Haipendezi na haionekani kuwa “professional” pale unapohitajika kutaja email address yako halafu ukatumia email yenye domain ya makampuni makubwa kama gmail, yahoo au Hotmail. Kama kampuni yako ni ABC Limited, basi ni vema ukasema jinalako@abc.com au jinalako@abc.co.tz